Arsenal yatinga top four EPL

0
135

Arsenal imepanda mpaka nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu ya England baada ya kuibanjua West Ham United mabao mawili kwa nunge katika mchezo wa ligi hiyo ulipigwa katika dimba la Emirates usiku wa kuamkia leo.

Gabriel Martinelli aliifungia Arsenal bao la kwanza mapema katika kipindi cha pili kabla ya kinda Emile Smith Rowe hajaingia kutoka benchi na kuwafungia Gunners bao la pili.

Nahodha mpya wa Arsenal Alexandre Lacazette alikosa penati ambayo iliokolewa na mlinda mlango wa West Ham Lukasz Fabianski.

Katika mchezo huo mchezaji wa West Ham Vladimir Coufal alitolewa nje baada ya kuoneshwa kadi ya pili ya njano latika mchezo huo ambao ulizikutanisha timu zote za mji waLondon (London Deby).