Al Hilal yaweka bilioni 816 mezani kumpata Mbappe

0
241
PARIS, FRANCE - DECEMBER 28: Kylian Mbappe of PSG celebrates his winning goal at 2-1 on a penalty kick during the Ligue 1 match between Paris Saint-Germain (PSG) and RC Strasbourg Alsace (RCSA) at Parc des Princes stadium on December 28, 2022 in Paris, France. (Photo by Jean Catuffe/Getty Images)

Al Hilal ya Saudi Arabia imetenga dau lililoweka rekodi ya dunia la TZS Bilioni 816.5 kwa ajili ya kunasa saini ya mshambuliaji wa Ufaransa na PSG, Kylian Mbappe (24).

Nahodha huyo wa Ufaransa ambaye bado ana mwaka mmoja kwenye mkataba wake na PSG hadi mwaka 2024 amekataa kuongeza mkataba wa kuwatumikia mabingwa hao wa Ufaransa.

Kutokana na mvutano huo, Mbappe hakujumuishwa kwenye kikosi cha maandalizi ya msimu ujao kilichokwenda Japan.

Pande hizo mbili zimekuwa kwenye mvutano ambapo PSG wanataka kumuuza sasa hivi, badala ya kumwacha aondoke bure mwakani pindi mkataba wake utakapoisha.

Hata hivyo, Mbappe anataka kuendelea kubaki PSG hadi mkataba wake utakapoisha ambapo inaaminika kuwa anataka kujiunga na Real Madrid wakati ukifika.

Mwenyekiti wa PSG, Nasser Al-Khelaifi ameweka wazi kuwa haiwezekani Mbappe akaruhusiwa kuondoka bure msimu ujao na kwamba kama anataka kubaki, lazima aongeze mkataba.