Al Ahly yamfuta kazi kocha wake

0
204
Martin Lasarte

Miamba ya soka nchini Misri, timu ya Al Ahly imemfuta kazi kocha wake Martin Lasarte , ikiwa ni siku moja baada ya kufungwa na kuondoshwa kwenye michuano ya Egypt Cup.

Al Ahly walifungwa bao moja kwa bila na matajiri wapya kwenye soka la Misri,timu ya Pyramids siku ya Jumamosi na hali iliyosababisha waondoshwe kwenye hatua ya 16 bora ya michuano hiyo ya Egypt Cup, kitu ambacho kiliwachefua matajiri wa timu hiyo ya jijini Cairo.

Kocha huyo Mruguay alierithi mikoba ya kocha Mfaransa Patrice Carteron,amefukuzwa kazi pamoja na kwamba aliisaidia timu hiyo kutwa ubingwa wa ligi kuu ya Misri msimu uliopita.

Baada ya Martin Lasarte kufukuzwa, Msaidizi wake Mohamed Youssef ataiongozatimu hiyo kwa muda huku akitafutwa kocha wa kigeni kuchukua nafasi ya kuwa kocha mkuu mpya wa timu hiyo yenye historia ndefu kwenye soka la Misri na Afrika kwa ujumla.