Al Ahly mabingwa wa Afrika kwa mara ya 11

0
200

Timu ya Al Ahly SC ya Misri imefanikiwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika licha ya sare ya 1-1 na wenyeji Wydad Athletic Club waliokuwa wanashikilia taji hilo.

Wydad walitangulia na bao la beki wake Yahya Attiat-Allah El Idrissi dakika ya 27, kabla ya Mohamed Abdelmonem kuisawazishia Al Ahly dakika ya 78.

Al Ahly wanabeba kombe kwa ushindi wa jumla wa 3-2, kufuatia kuwachapa Wydad 2-1 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita jijini Cairo na hilo linakuwa taji la 11.