Klabu ya soka ya Simba imemtangaza aliyekuwa mtangazaji wa kituo cha Runinga cha Azam Tv, Ahmed Ally kama Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo kuanzia leo Januari 3,2022.
Simba kupitia kurasa rasmi za klabu hiyo imeweka picha na kuandika “ Karibu Ahmed Ally, New Media and Communication Manager”
Taarifa hiyo imemuelezea Ahmed kama ni kijana mchapakazi, mwenye uhusiano mzuri na watu wa aina zote, mtanashati na kubwa zaidi mapenzi yake kwa Simba hayapimiki.
“Ahmed Ally karibu kwenye klabu ya maisha yako kuwatumikia Wanasimba kama Afisa Habari na Mawasiliano”-imeeleza taarifa ya Simba