Ahamed Ally: Wachezaji Simba wanadai bonus za michezo ya nyuma

0
1140

Afisa Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema ni kweli kuwa wachezaji wa timu hiyo wanadai posho zao za michezo ya nyuma, lakini hiyo siyo sababu ya kufungwa katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

“Ni kweli wachezaji wanadai posho zao na hilo ni jambo la kawaida, kuna wakati taasisi inakuwa na fedha na inalipa madeni yote, na kuna wakati taasisi inakosa fedha inalimbikiza madeni, mzigo ukipatikana inamaliza,” amesema Ally.

Amesema kuwa ikifika hatua kuwa mchezaji hataki kucheza hadi alipwe posho yake, hapo itawabidi waulizane mara mbilimbili, huku akithibitisha kuwa watalipwa fedha zao.

Baada ya kutolewa ASFC amesema timu hiyo imezomewa kutoka Mtwara hadi Dar es Salaaam hali ambayo inawaumiza zaidi wachezaji.

“Hakuna mchezaji anayetaka kufungwa makusudi ili azomewe kuzomewa ni kitendo cha aibu sana,” ameeleza.