76’ERS mbabe kwa Brooklyn Nets

0
537

Joel Embiid amefunga alama 39 na kucheza mipira iliyorudi 13 na kuisaidia timu yake ya Philadelphia 76’ERS kuibuka na ushindi wa alama 123 kwa 110 dhidi ya Brooklyn Nets kwenye Ligi Kuu ya Mpira wa Kikapu nchini Marekani (NBA).

Licha ya Joe Harris kuifungia Nets alama 22,  bado hazikutosha kuwapa ushindi mbele ya Sixers ambao ushindi huo unakuwa wa 48 kwao kwa msimu huu wakiwa tayari wamejihakikishia nafasi ya kucheza hatua ya mtoano yaani Play Off.

Katika matokeo mengine,  wakongwe Miami Heat wamepanda hadi katika nafasi ya Nane kwenye msimamo wa Kanda ya Mashariki baada ya kuibuka na ushindi wa alama 105 kwa 99 dhidi ya Dalas Mavericks katika mchezo ambao Goran Dragic ameifungia Heat alama 23 na kucheza michezo iliyorudi yaani Rebounds 12.

Orlando Magic wameporomoka hadi katika nafasi ya Tisa kwenye msimamo wa kanda hiyo baada ya kukubali kipigo cha alama 115 kwa 98 kutoka kwa Detroit Pistons na sasa wana kazi ya ziada kupambana kurejea katika nafasi ya Nane ambayo imekaliwa na Miami Heat ili kufanikiwa kucheza hatua ya Play Off.

Huko Taxas,- James Harden ameendeleza moto kwa kufunga alama 38 na kuisaidia Huston Rockets kupata ushindi wa alama 112 kwa 85 dhidi ya Denver Nuggets wakati New York Knicks wakishindwa kutamba mbele ya Toronto Raptors na kukubali kipigo cha alama 117 kwa 92 huku Milwaukee Bucks wakiinyuka Los Angeles Clippers alama 128 kwa 118.