Njia 10 za kukuwezesha kupunguza uzito

0
367

Najua huenda mwaka 2021 lengo lako lilikuwa kupunguza uzito lakini hukufanukiwa, basi tulihamishie lengo hilo mwaka 2022, na hapa tutazileta njia 10 rahisi kukuwezesha kufikia lengo hilo.

Kupunguza uzito linaweza kuwa jambo gumu au jepesi kulingana na muhusika mwenyewe. Lakini kufanikisha, hakikisha unakuwa na msimamo na mwendelezo katika yale unayofanya, hata kama ni madogo kiasi gani.

Epuka kula kila mara
Ulaji wa kila mara hasa wa vitafunwa kunapelekea mtu kula chakula kingi na mara nyingi vinakuwa vyenye kiwango kikubwa cha sukari. Kama unahisi njaa, kula chakula chenye protini nyingi ili kukusaidia kuhisi umeshiba.

Usinywe vinywaji vya sukari
Hivi vinaongeza kiwango cha kalori ndani ya mwili wako, hivyo ni muhimu kuviepuka, na kutumia mara tu unapohitajika sana. Badala yake kunywa maji.

Milo mitatu kwa siku
Kiwango cha juu zaidi cha chakula unachotakiwa kula ni milo mitatu kwa siku, ukiweza kula chini ya hapo ni bora. Ulaji sana unasababisha kuongeza uzito

Kula taratibu

Kwa wastani inamchukua mtu dakika 20 kuweza kutambua kama ameshiba, hivyo ukila haraka, unaweza kula chakula kingi kuliko ulichohitaji. Ukila taratibu utaweza kuhisi unavyoshiba, na ukifika 80% ya tumbo lako, unashauriwa kuacha kula.

Kula protini
Protini inafanya mambo matatu yanayokusaidia kupunguza uzito;

  1. Unakufanya ujihisi kushiba kwa muda mrefu
  2. Inameng’enywa kwa urahisi kuliko wanga na fat.
  3. Inahifadhi misuli (lean muscle)

Kula vyakula vya kukusaidia

  1. Mboga majani zenye nyuzi nyuzi
  2. Nyama
  3. Vyakula vya fat
  4. Matunda yenye kiwango kidogo cha sukari
  5. Viazi ulaya na mizizi mingineyo.

Punguza sukari iliyochakatwa
Kuna faida kubwa sana ya kupunguza ulaji wa vyakula vyenye sukari iliyochakatwa, kwani watu wanaofanya mazoezi hufanya hivyo kuchoma sukari ndani ya miili yao.

Punguza au epuka soda, chai, juisi za viwandani, kahawa zenye sukari, chokoleti.

Fanya mazoezi
Kuna aina mbalimbali za mazoezi unayoweza kuyafanya ikiwa ni pamoja na kukimbia, kuruka kamba, kucheza muziki, kubeba vitu vizito walau dakika 30 hadi 45 kwa siku na wala mara tatu kwa wiki.

Tumia Kafeini
Kazi kubwa ni kukusaidia kupunguza hamu ya kula na kuimarisha uwezo wako wa kusaikolojia. Kama hupendi kahawa unaweza kutumia chokoleti nyeusi au chai nyeusi ambazo zote zina kafeini.

Kuwa na mpangilio wa kula
Hakikisha unakuwa na utaratibu wa kujua ni wakati gani unatakiwa kula chakula, usiwe mtu wa kula kila mara unapokutana na chakula.