Zungu ataka wabunge kuacha kuomba miongozo isiyo na maana

0
134

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Zungu amekemea tabia za baadhi ya wabunge kusimama na kuomba miongozo wakati wenzao wakichangia, huku wanachokizungumza kikiwa hakina maana.

Amesema tabia hiyo ni sawa na kuwaondoa wachangiaji kwenye mstari na kutaka tabia hiyo isijitokeza wakati bunge litakapojadili mjadala wa bajeti kuu ya serikali inayotarajiwa kuwasilishwa bungeni hapo kesho.

Zungu ametoa kauli hiyo bungeni jijini Dodoma mara baada ya kipindi cha maswali na majibu.

Amesema taarifa nyingi zinazotolewa na Wabunge huwa si za msingi zaidi ya kuharibu mtiririko wa wachangiaji na ni
utovu wa nidhamu hata kwa kiti ambacho kinaongoza kwa wakati huo.