Wanafunzi wa shule ya msingi Mikocheni A iliyopo mkoani Dar es Salaam, wakishiriki kampeni ya kupanda miti ili kutunza mazingira.
Kampeni hiyo maalum imeandaliwa na Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na ina lengo la kuunga mkono juhudi za serikali katika utunzaji wa mazingira.