ZANZIBAR YAIMARISHA MIFUMO YA HUDUMA ZA MTANDAO

0
147

Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wamehimizwa kuendelea kutumia huduma za mawasiliano na kutoa huduma kwa Wananchi kwa kutumia mifumo ya Serikali mtandao, ili kurahisha utendaji kazi na huduma kwa jamii.

Wito huo umetolewa Zanzibar na Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Rais Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini Josephine Kimaro baada ya kusaini mkataba wa huduma ya mtandao kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia wakala wa Serikali Mtandao (eGAZ) na kampuni ya Vodacom Tanzania.

Ushirikiano huo utajumuisha mifumo ya mitandao na kidigitali na kuendelea kuifanya Zanzibar kuwa moja ya maeneo muhimu kwa utalii Tanzania.