Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeanza mkakati wa kupata viwanda vya kuteketeza taka hatarishi ili kuendelea kuweka mazingira safi na kuimarisha Utalii visiwani humo
Akizungumza wakati wa ziara ya kamati ya kusimamia viongozi wakuu wakitaifa Zanzibar, Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Saada Mkuya Salum amesema lengo kubwa la ziara hiyo ni kujifunza na kufanya tafiti kabla ya kuanza mradi huo Tanzania Zanzibar
Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti Mtumwapea Yusuph imefanya ziara katika mikoa ya Dar es salaam na Pwani na kutembelea Tume ya Dawa za kulevya pamoja na mradi wa uchomaji taka hatarishi wa TMHS uliopo Kisarawe mkoani Pwani
