Vijiji saba vinavyozunguka hifadhi ya Akiba ya Lukwati /Piti katika wilaya ya Songwe na Chunya vimenufaika na utalii wa uwindaji baada ya kujengewa zahanati na shule kutokana na asilimia 25 % ya mapato yanayotokana na uwindaji huo.
Wananchi hao kutoka Vijiji vya Ngwala ,Itiziro ,Kapalala na Gua katika Mikoa ya Mbeya na Songwe wamesema kujengwa kwa miradi hiyo hususani zahanati na shule kumesaidia kuondoa kero za muda mrefu kwa wananchi kutembelea umbali mrefu kufuata huduma hizo muhimu katika maeneo mengine.
Meneja wa pori ,Jembe Grispo kutoka mamlaka ya usimamizi wanyama pori Tawa anaelezea umuhimu wa pori hilo kwa wananchi.
Taarifa ya misaada hiyo imeungwa mkono na wakurugenzi wa halmashauri ya Chunya Sophia Kumbuli na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Songwe Fauzia Hamidu.