Serikali imeandaa programu mbalimbali za kutunza mazingira, ikiwa ni pamoja na ile ya kupanda miti zaidi ya Bilioni Moja katika eneo la Mlima Kilimanjaro ili kukabiliana na mabadiliko ya Tabia Nchi.
Akijibu swali Bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, -Mussa Zungu amesema kuwa lengo la kupanda miti hiyo ni kulinda barafu iliyopo katika eneo hilo.
Waziri Zungu ameongeza kuwa, programu hiyo ya kupanda miti na kuitunza itafanyika pia katika wilaya zote nchini na itapandwa aina ya miti inayoendana na mazingira ya wilaya husika.