Zaidi ya kilo 300 za dawa za kulevya zakamatwa

0
496

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imewakamata watuhimiwa watatu wakiwa na kilo zaidi ya 300 za dawa za kulevya aina ya mirungi na gramu 448 za heroini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, James Kaji amesema watuhumiwa hao raia wa Tanzania wamekamatwa katika maeneo ya Dar es Salaam na mkoa wa Kigoma wakijiandaa kusafirisha dawa hizo kwa njia ya posta kwenda Ulaya.