Yanga yamtupia virago Nugaz

0
619

Klabu ya soka ya Yanga imetangaza kuacha na aliyekuwa afisa mhamasishaji wa klabu hiyo Juma Nugaz Maarufu Antonio Nugaz kuanzia hii leo Septemba 1, 2021.

Taarifa ya klabu hiyo iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga imeeleza kuwa Nugaz amemaliza mkataba wake ndani ya Yanga na kwamba wanamtakia kila la kheri katika Maisha yake nje ya klabu hiyo.

“Juma (Nugaz) amaemaliza mkataba wake wa utumishi wa miaka miwili ndani klabu ya Yanga, hivyo uongozi umeamua kutoongeza mkataba na kwamba unamshukuru sana kwa kazi yake na kumtakia kila la kheri na mafanikio katika maisha na kazi zake nje ya klabu ya Yanga,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo

Klabu ya soka ya Yanga ipo katika mchakato wa kuboresha uendeshaji wake ambapo hivi karibuni imemtangaza Senzo Mbatha kuwa Afisa mtendaji mkuu wa mpito ikiwa ni hatua za kuingia katika mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo.