Wizara ya Maliasili na Utalii kuendelea kushirikiana na Wasanii kutangaza Utalii

0
225

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, -Constantine Kanyasu, amewapongeza Wasanii nchini kwa kuonyesha utayari wa kushirikiana na Wizara hiyo katika kunadi vivutio vya Utalii nchini.

Akizungumza na Wasanii mbalimbali pamoja na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam, -Naibu Waziri Kanyasu amesema kuwa, kazi ya sanaa nchini inakua kwa kasi, hivyo Wasanii hawawezi kuachwa nyuma katika kutangaza na kuhamasisha Utalii.

Amewahakikishia Wasanii nchini kuwa, Wizara ya Maliasili na Utalii ipo tayari muda wowote  kutoa ushirikiano kwa Msanii yeyote atakayetaka kufanya kazi na Wizara hiyo.

Mkutano huo uliwakutanisha  Wasanii mbalimbali wakiwemo wale wa filamu, vichekesho, uchongaji pamoja washindi wa Miss Utalii kwa miaka minne iliyopita.