Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Kilimo kuhakikisha inawasimamia ipasavyo Mawakala waliopewa kazi ya kusambaza pembejeo za kilimo na Mbegu, ili waweze kufanya kazi hiyo kwa wakati na kwa bei iliyopendekezwa.
Waziri Mkuu Majaliwa ametoa agizo hilo wakati akiahirisha mkutano wa 16 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma.
Amesema kuwa wizara ya Kilimo inatakiwa kuwasimamia Mawakala hao ili waweze kupeleka kwa Wakulima pembejeo za kilimo na mbegu kwa Wakulima kwa wakati na hasa kipindi hiki cha kuelekea kwenye maandalizi ya msimu wa mvua za Vuli.
Hata hivyo Waziri Mkuu ameitaka Wizara hiyo ya Kilimo kuratibu kwa karibu bei ya pembejeo na mbegu kwa Wakulima ili ziwe ni zile zilizopendekezwa na serikali na si vinginevyo.
Waziri Mkuu Majaliwa ameliahirisha Bunge hadi Novemba Tano mwaka huu.