Wizara ya Kilimo yaagizwa kuimarisha vyuo vya utafiti

0
311

Wizara ya Kilimo imetakiwa kuweka bajeti kubwa katika suala zima la utafiti ili kuimarisha vyuo vya utafiti nchini ambavyo vina mchango mkubwa katika kuleta mapinduzi ya kilimo nchini.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hayo baada ya kutembelea Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha TARI Naliendele mkoani Mtwara ambapo ameridhishwa na kazi zinazofanyika katika kituo hicho.

Majaliwa amesema Kituo cha Naliendele kimekuwa kikifanya kazi kubwa ya utafiti wa mbegu bora za korosho nchini na sasa wanafanya utafiti wa mazao mengine ya mafuta na mikunde.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti nchini, Dkt. Geofrey Mkamilo anasema licha ya kazi kubwa ya utafiti wanayoifanya, kituo hicho ni chakavu hivyo serikali ikiangalie kwa jicho la huruma.

Serikali imeendelea kuboresha mazao mbalimbali ya kilimo nchini ambapo ilianza na mazao matano ya kimkakati ambayo ni korosho, chai, tumbaku, kawaha na pamba ambapo kwa sasa imeongeza mazao mengine ya mafuta kama vile karanga na michikichi ili kuleta tija kwa wakulima.