Wizara ya afya yatangaza ongezeko la wagonjwa wapya 84 wa Corona

0
745

Wizara ya afya nchini Tanzania imetangaza ongezeko la wagonjwa wapya 84 wenye maambukizi ya virusi vya corona.

Kati ya wagonjwa hao, 16 ni wagonjwa waliotolewa taarifa na waziri wa afya visiwani Zanzibar leo Aprili 20, 2020.

Ongezeko la wagonjwa wapya linafanya idadi ya watu waliopata maambukizi ya ugonjwa wa corona nchini kufikia 257 kutoka wagonjwa 147 waliotolewa taarifa Aprili 17 mwaka huu.

Aidha, watu watatu waliothibitika kuambukizwa COVID-19 wamefariki dunia jijini Dar es Salaam.