Wivu wa kimapenzi wasababisha kifo

0
159

Jeshi la polisi mkoani Tanga linamshikilia Mashaka Bakari mkazi wa Handeni, kwa kosa la kumuua mtalaka wake kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa polisi wa mkoa wa Tanga Blasius Chatanda amesema, mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Agosti 20 mwaka huu majira ya saa tatu usiku kwa kutumia silaha aina ya gobole.

Katika hatua nyingine Kamanda Chatanda amesema Jeshi la polisi mkoani Tanga limekamata watoto 60 wenye umri wa kati ya miaka 9 na 15 maarufu kwa jina la watoto wa Ibilisi, ambapo 20 kati yao wamehukumiwa kifungo jela.

Amesema watoto hao wamekua wakizunguka katika mitaa ya jiji la Tanga, na kufanya uhalifu wa kupora raia vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na simu na pesa.

Kwa mujibu wa Kamanda Chatanda, watoto hao wamekuwa wakitumua nyembe, mapanga na bisibisi kufanya uhalifu huo.