Wiki ya Maziwa: Watanzania waaswa kutumia maziwa ya ndani ya nchi

0
543

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega ametoa wito kwa viongozi, taasisi, makampuni, wizara na wananchi kutumia maziwa yanayozalishwa hapa nchini ili kukuza uchumi wa taifa letu.

Ulega ametoa wito huo jijini Dodoma katika Maadhimisho ya Wiki ya Maziwa mwaka 2020 na kuongeza kuwa serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wazalishaji wa maziwa nchini.

Katika hali ya kusikitishwa, amesema ofisi mbalimbali za serikali maziwa yanayotumika ni ya unga, hivyo amewataka Watanzania kuwa wazalendo kwa kupenda vya kwetu, na kwamba ni aibu watumishi wa umma kutumia maziwa ya unga.

“Ni lazima tuchukue hatua za makusudi kama kweli tunataka kweli kuhakikisha nchi yetu inasonga mbele, kwa kuamua kabisa kutumia bidhaa za ndani, hasa maziwa yanayozalishwa na viwanda vyetu,” amesema Ulega

Sekta ya mifugo nchini Tanzania inachangia asilimia 7 katika Pato la Taifa (GDP), lakini ndani ya asilimia hiyo, asilimia 1.2 inatokana na maziwa.