Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akivalishwa vazi la kuwa kiongozi wa jamii ya Kimasai na Laighwanani Mkuu wa Jamii ya Wamaasai Tanzania Isack Ole Kisongo Meijo, mara baada ya kuwasili katika eneo la Mto wa Mbu wilaya ya Monduli mkoani Arusha leo Mei 16, 2023.
Dkt. Mpango yupo mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya ufunguzi wa barabara ya Mto wa Mbu – Loliondo sehemu ya Wasso – Sale yenye urefu wa Kilomita 49.