Wenyeviti wa vijiji waonywa kuhusu ardhi

0
251

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amewaonya Wenyeviti wa vijiji katika maeneo mbalimbali nchini wanoendelea  kutoa ardhi zaidi ya ekari Hamsini kwa wawekezaji kinyume na mamlaka yao.

Waziri Lukuvi ametoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko ya Wakazi wa kijiji cha Mbuyuni kilichopo wilayani Iringa ambapo kuna nwekezaji aliyepatiwa ekari 180 na uongozi wa kijiji kinyume cha sheria.

Ameeleza kushangazwa na hatua ya uongozi wa kijiji hicho cha Mbuyuni kukaidi agizo la serikali na kutoa ardhi hiyo.