Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema atahakikisha Samaki wanaovuliwa katika Mwalo wa Chato mkoani Geita wanapata soko la uhakika nchini China kutokana na ubora walionao.
Waziri Wang Yi ametoa ahadi hiyo baada ya kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa katika Mwalo huo akiwa katika siku ya pili ya ziara yake hapa nchini.
Naye Waziri wa MIfugo na Uvuvi Mashimba Ndaki, ameiomba Serikali ya China kusaini mkataba utakaosaidia Mabondo ya samaki aina ya Sangara yanapata soko nchini humo.
Ziara ya Waziri Wang Yi hapa nchini iliyoanza hapo jana, inahitimishwa hii leo.