Waziri wa Mambo ya Nje wa China kufanya ziara Tanzania

0
173

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi amesema mtazamo wa Tanzania kwa Bara la Afrika ni kuona linajitegemea kwa kutumia rasilimali zake kufanya maendeleo.
 
Waziri Kabudi ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wake na Waandishi wa habari, ambapo pamoja na mambo mengine amezungumzia ujio wa Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi Januari 7 mwaka 2021.

Ziara ya siku mbili ya Wang Yi hapa nchini, ni muendelezo wa uhusiano wa muda mrefu baina ya Tanzania na China.