Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. PALAMAGAMBA KABUDI amekagua pikipiki ambazo zitatumika kuongoza misafara ya Marais na wakuu wa serikali watakaohudhuria mkutano huo wa 39 wa SADC.
Prof. KABUDI amesema ameridhishwa na maandalizi mbalimbali ya mapokezi ya viongozi hao ikiwa ni pamoja na vyombo vya usafiri ikiwemo magari na pikipiki achilia mbali hotel watakazofikia viongozi hao.
Aidha Prof. KABUDI ameeleza kuridhishwa na namna vyombo vya habari nchini vinavyoripoti kizalendo Mkutano wa SADC unaoendelea akisema vimesaidia kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu SADC.
Katika tukio jingine Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. KABUDI amepokea nakala ya hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa DENMARK hapa nchini METTE NORGAARD DISSING-SPANDET.