Waziri Ndalichako atoa Onyo

0
214

Serikali imesema katika mwaka wa masomo wa 2019 /2020 wanafunzi wote wa elimu ya juu waliofuata masharti na vigezo vilivyowekwa ili kupata mkopo wamepatiwa fedha hiyo.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof, JOYCE NDALICHAKO amewaeleza waandishi wa habari Mkoani KIGOMA kuwa katika mwaka wa fedha 2019 /2020 serikali kupitia bunge ilitenga shilingi BILIONI MIANNE NA HAMSINI ikilenga kutoa mikopo kwa wanafunzi ELFU AROBAINI NA TANO wa mwaka wa kwanza na kwamba hadi kufikia mwezi Novemba mwaka huu tayari imetoa shilingi BILIONI MIA MBILI Na MBILI sawa na asilimia AROBAINI NA TANO ya fedha yote iliyotengwa kwa ajili ya mikopo hiyo.