WAZIRI NAPE:TEHAMA ISIHARIBU UTAMADUNI WETU

0
146

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amewataka Watanzania kutumia mitandao ya kijamii kuondoa chuki na si kudhalilishana, jambo ambalo sio utamaduni wa Mtanzania.

Waziri Nape ameyasema hayo wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro wakati wa hafla ya kuwapongeza waliofanikisha huduma ya data katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Nape amesema iko haja ya kutumia mitandao ya kijamii kupeleka heshima mahali ambapo watu wameanza kudharauliana.

” Tehama lazima iturudishie heshima isiwe chanzo cha kuharibu utamaduni wetu”, amesema Nape.

Amesema sheria zipo na Serikali haitasita kuwachukulia hatua wale wote watakaotumia vibaya mitandao ya kijamii kutukanana.