Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Mawasiliano wa Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU) Doreen Bogdan-Martin
pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa Maendeleo ya Mawasiliano Duniani (ITU-WTDC-2022) jijini Kigali, Rwanda.
Miongoni mwa ajenda nyingine wamejadili namna ya kuiwezesha Tanzania kuboresha miundombinu ya Usalama Mtandaoni kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania. pamoja na kuboresha TEHAMA mashuleni na kwa wasichana kupitia programu bayana za ITU.