Waziri Mwinyi aanza ziara Mara

0
187

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein amewasili mkoani Mara kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili, ambapo pamoja na mambo mengine atatembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa -SUMA JKT.

Akitoa taarifa kwa Waziri Mwinyi, Mkuu wa mkoa wa Mara, -Adam Malima amesema kuwa, uwepo wa JKT mkoani humo, umesaidia kukuza uchumi wa mkoa huo, kwa kuwa Jeshi hilo limekua likitekeleza miradi mbalimbali ambayo ni pamoja na ile ya ufugaji wa samaki na kilimo.