Waziri Mkuu ziarani nchini Burundi

Ziara ya siku moja nchini Burundi

0
187

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amewasili nchini Burundi ambapo anafanya ziara ya siku moja nchini humo.

Katika uwanja wa ndege wa Bujumbura, Waziri Mkuu Majaliwa amepokelewa na Makamu wa Rais wa Burundi, Prosper Bazombanza.

Miongoni mwa malengo ya ziara hiyo ya Waziri Mkuu nchini Burundi ni kuimarisha uhusiano wa Tanzania na Taifa hilo.