Waziri Mkuu : Tupo tayari kuwatumikia Watanzania

0
254

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuahidi Rais Samia Suluhu Hassan kuwa yeye pamoja na Mawaziri na Naibu Mawaziri wote watafanya kazi kwa nguvu zao zote katika kuwatumikia Watanzania.

Akizungumza Ikulu Chamwino mkoani Dodoma wakati wa hafla ya kumuapisha Katibu Mkuu Kiongozi, Mawaziri 8 na Naibu Mawaziri 8, Waziri Mkuu Majaliwa amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kumuamini na kumbakiza katika nafasi hiyo.

Amemueleza Rais kuwa yupo tayari  kupokea maelekezo kutoka kwake na Mawaziri na Naibu Mawaziri  wote alioweateua wapo tayari kupokea maelekezo na kuchapakazi.

Waziri Mkuu Majaliwa amewatoa mashaka Watanzania kwa kusema kuwa Mawaziri wote wapo tayari kuwatumikia na kuwahudumia.