Waziri Mkuu : Tumieni vyombo vya habari kutoa elimu

0
115

bari katika ngazi ya kitaifa na wilaya kutoa elimu kwa watumiaji wa vyombo vya moto na barabara, ili kudhibiti ajali nchini.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa licha ya baadhi ya vyombo vya habari kutoa elimu kwa umma kikiwemo kipindi cha Usalama Barabarani na Uraia (UBU) kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), lakini elimu hiyo inapaswa kutolewa zaidi kwenye kila ngazi.

Amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dkt. Ayub Rioba Chacha kuhakikisha elimu zaidi inatolewa na TBC kuhusu matumizi ya barabara na sheria za usalama barabarani.

“Bahati nzuri Mkurugenzi Mkuu wa TBC yupo hapa na yeye ni mjumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, nakuagiza kusimamia suala la utoaji elimu ya usalama barabarani kwa kutumia vyombo vya habari.” amesisitiza Waziri Mkuu Majaliwa

Kipindi cha UBU kinarushwa na shirika la Utangazaji Tanzania na kinatoa elimu ya usalama barabarani na uraia.