Waziri Mkuu: Mwalimu Nyerere atakumbukwa kwa ujenzi wa taifa

0
226

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema, Baba wa taifa mwalimu Nyerere atakumbukwa kwa ujenzi wa Taifa imara lenye umoja na mshikamano na fikra zake zitaendelea kuishi

Akizungumza wakati wa mdahalo wa Kitaifa wa Kuadhimisha miaka 100 ya Kuzaliwa kwa Mwalimu Nyerere, uliofanyika katika shule ya uongozi ya Mwalimu Nyerere, Kibaha Mkoani Pwani, Waziri Mkuu amesema siku zote mwalimu atakumbukwa kwa ujenzi wa Taifa imara

Mdahalo huo umehudhuriwa pia na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan