Waziri Mkuu Majaliwa: Serikali haina dini

0
216

Licha ya dini kuwa na mchango mkubwa wa kuchochea amani nchini Tanzania, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa serikali haina dini, lakini watu wake wana dini.

Amesema kwa kutambua hilo, serikali imeendelea kuweka mazingira rafiki yanayotoa nafasi kwa kila mmoja kusali kulingana na imani yake.

Akizungumza katika mkutano na Viongozibwa Dini unaoangazia amani kuelekea Uchaguzi Mkuu, Majaliwa ameongeza kuwa maombi ya viongozi wa dini ndiyo yaliyoiepusha na majanga mbalimbali yakiwamo nzige wavamizi na virusi vya corona.

Amewashukuru viongozi hao kwa kumuunga mkoni Rais Dkt. Magufuli pamoja na mambo aliyoyafanya katika ustawi wa amani, uzalendo na kumtanguliza Mungu, huku akiwahakikishia kwamba, serikali itaendeleza mshikamano huo kwa manufaa ya Watanzania wote.