Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuongoza mazishi ya Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, – Dkt Reginald Mengi yatakayofanyika kesho Alhamisi Mei Tisa kijijini kwake Kisereni, Machame wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
Waziri Mkuu ataongoza mazishi hayo kwa niaba ya Serikali ambapo Ibada ya mazishi itafanyika kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) la Kisereni, Machame.
Tayari mwili wa Dkt Mengi ambaye alifariki dunia Mei 2 mwaka huu huko Dubai, umewasili mkoani Kilimanjaro ukitokea jijini Dar es salaam na kupokelewa na mamia ya wakazi wa mkoa huo.
