Waziri Mkuu kumwakilisha Rais Magufuli Russia

0
299

Mkutano wa siku Mbili wa Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka Mataifa ya Afrika na Russia (Russia – Africa Summit) umepangwa kufanyika Oktoba 23 na 24 mwaka huu katika mji wa Sochi nchini Russia.

Katika mkutano huo Tanzania inawakilishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa niaba ya Rais John Magufuli.
 
Mkutano huo utakaoendeshwa chini ya Uenyekiti wa pamoja wa Rais Vladimir Putin wa Russia na Rais Abdel Fattah El-Sisi wa Misri ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), unalenga kurejesha na kuimarisha uhusiano baina ya Mataifa ya Afrika na Russia, uhusiano ambao uliyumba miaka ya 1990.
 
Tayari Waziri Mkuu Majaliwa na Ujumbe wake ameondoka nchini, kuelekea Russia.