Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezipongeza klabu za Simba na Yanga kwa kutinga hatua ya makundi katika mashindano ya ngazi ya klabu Barani Afrika.
Akisoma hotuba ya kuahirisha mkutano wa tisa wa Bunge Bungeni jijini Dodoma, Waziri Mkuu Majaliwa amesema Serikali inazipongeza timu hizo kwa kufanikiwa kutinga hatua ya makundi katika Klabu Bingwa Barani Afrika na Kombe la Shirikisho mtawalia.
“Nazipongeza klabu zetu kwa kufanya vizuri katika mashindano ya Afrika na kutinga hatua ya makundi. Kwa Simba wao wametinga hatua ya makundi katika Ligi ya Mabingwa Barani Afrika na Yanga kombe la Shirikisho.” amesema Waziri Mkuu na kuongeza kuwa
“Kipekee naipongeza klabu ya Yanga kwa kuibuka na ushindi wa kihistoria dhidi ya timu za Afrika Kaskazini na kuingia kwa kishindo hatua ya makundi katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika.”