Waziri Mkuu azindua Punje ya Tumaini

0
171

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezindua kitabu cha Riwaya chenye jina la Punje ya Tumaini kilichoandikwa na mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC Elizabeth Mramba kilichobeba maudhui ya yenye simulizi ya madhara ya dawa za kulevya

Waziri Mkuu amezindua kitabu hicho kwenye kilele cha maadhimisho ya Kitaifa ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani ambapo kitaifa imefanyika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam huku akitaka Jamii kuendelea kupiga vita dhidi ya dawa za kulevya.

Waziri Mkuu Majaliwa amewaasa wanasiasa kutumia nafasi zao kuelimisha Jamii juu ya madhara ya dawa za kulevya huku akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha inaongoza mapambano dhidi ya matumizi ya dawa hizo

Aidha Elizabeth Mramba amesema ameamua kuandika kitabu hicho ikiwa ni mchango wake kwa Jamii Katika kutoa elimu ya madhara ya dawa za kulevya akilenga elimu hiyo kuwafikia vijana wakiwa bado wadogo kabla hawajaathirika na dawa hizo.

“Riwaya hii inaionesha jamii kwamba lipo tumaini kwa waathirika au waraibu wa dawa za kulevya kwamba wanaweza kutibiwa kwanye vituo vya afya ama kwenye nyumba za upataji nafuu (sober houses) na wakapona na kurejea katika maisha ya kawaida” ameongeza Elizabeth

Kila tarehe 2 mwezi wa Julai Dunia huadhimisha siku ya kupinga matumizi ya dawa za kulevya ambapo Tanzania imeadhimishwa Kitaifa Mkoani Dar es Salaam ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Kasimu Majaliwa huku maadhimisho ya Mwaka huu yakiongozwa na kauli mbiu ya “Tukabiliane na changamoto za dawa za kulevya kwa Ustawi wa Jamii”