Waziri Mkuu aunguruma Jijini Tanga, asisitiza uwajibikaji kwa viongozi

0
175

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka viongozi, wakuu wa idara na watumishi wa umma kufanya kazi kwa ushirikiano na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma

Aidha Waziri Mkuu amesema serikali itaendelea kuboresha na kuhakikisha wakulima wanapata faida kwa kile wanachokizalisha

Akizungumza katika ziara yake mkoani Tanga amesema serikali itasimamia zao la katani ili kurudi katika ubora na kiwango chake katika uzalishaji na kutafuta masoko ya uhakika

Katika ziara hiyo mkoani Tanga Waziri mkuu Kassim Majaliwa amepokea taarifa ya kamati maalum aliyoiunda Novemba 2019 kufuatilia mali za mamlaka na bodi ya mkonge zilizokuwa mikononi mwa watu binafsi kinyume cha sheria