Waziri Mkuu aridhishwa na ujenzi wa machinjio

0
177

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameelezea kuridhishwa na kasi ya
ujenzi wa machinjio ya kisasa ya ng’ombe na mbuzi inayojengwa
katika eneo la Vingunguti jijini Dar es salaam.

Waziri Mkuu Majaliwa ameeleza hayo mara baada ya kukagua ujenzi
wa machinjio hiyo, wakati akifuatilia utekelezaji wa maagizo ya Rais John Magufuli.

Ujenzi huo wa machinjio ya kisasa ya ng’ombe na mbuzi katika eneo
la Vingunguti unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu.