Waziri Mkuu amuagiza DC kuboresha madawati

0
136

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Januari 25, 2022 amekagua ujenzi wa madarasa katika Shule ya Sekondari ya Kutwa Babati akiwa katika ziara ya mkoa wa Manyara.

Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Wilaya kusimamia maboresho ya madawati katika shule hiyo kwa kuweka ubao badala ya bati kama ilivyo sasa ili kuepusha madhara kwa watoto, bila kuathiri mwenendo wa masomo kwa wanafunzi.

Pia, Waziri Mkuu amewataka wazazi wote nchini kushirikiana na walimu kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri ya kitaaluma ili kila mtoto wa kitanzania wapate elimu bora