Waziri Mkuu afurahishwa na kazi za STAMICO

0
193

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ametembelea banda la Shirika la madini nchini STAMICO na kupongeza shughuli zijazofanya na Shirika hilo katika kuimarisha sekta ya madini.

Akiwa kwenye banda hilo katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam leo wakati wa Mkutano wa kimataifa wa uwekezaji kwenye sekta ya madini ameahidi kutembelea ofisi zao ili kuongeza ufanisi kwenye sekta ya madini.