Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, leo amefanya ziara kukagua mradi wa mabasi yaendayo haraka katika vituo vya Gerezani na Kariakoo mkoani Dar es salaam na kubaini dosari nyingi katika uendeshaji wa mradi huo.
Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu Majaliwa amemhoji Mkurugenzi wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (Dart) Mhandisi Ronald Lwakatare kwa nini mfumo wa ukusanyaji wa mapato unafanyika bila kutumia mifumo ya TEHAMA ambapo majibu yake yameonesha kutomridhisha.
Waziri Mkuu pia amejionea mabasi yaliyoharibika yakiwa kwenye karakana na kuhoji kwa nini hayafanyiwi marekebisho na badala yake vipuri vyake vinatolewa na kufungwa kwenye mabasi mengine, ambapo majibu ya wataalam yameonesha kutomridhisha.