Waziri Mkuu aanza ziara Morocco

0
135

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, leo amewasili nchini Morocco kwa ziara ya kikazi.
 
Katika uwanja wa ndege wa Mohammed V jijini Casablanca, Waziri Mkuu Majaliwa amepokelewa na Waziri Mwakilishi wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika wa Morocco, Mohcine Jazouli.
 
Lengo la ziara hiyo ya Waziri Mkuu Majaliwa nchini Morocco ni kuimarisha uhusiano hasa wa kiuchumi kati ya Tanzania na nchi hiyo.
 
Katika ziara hiyo Waziri Mkuu Majaliwa amefuatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor, Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda na Mkurgenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo, Japhet Justine.