Waziri Mkuu aagiza tamko kuahirishwa mechi ya watani wa jadi

0
295

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameiagiza wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoa tamko rasmi kwa Watanzania kuhusu hatua ya kuahirishwa kwa mchezo baina ya watani wa jadi Simba na Yanga.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa agizo hilo wakati wa mkutano wa tatu, kikao cha ishirini na sita Bungeni jijini Dodoma.

Amesema ni vema jambo hilo likatolewa tamko mapema ili kuondoa minong’ono inayoendelea kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na midomoni mwa Wananchi.

Mchezo wa Simba na Yanga ulitakiwa kuchezwa tarehe 8 mwezi huu katika uwanja wa Benjamin Mkapa mkoani Dar es salaam, lakini haukuchezwa baada ya kubadilishwa muda wa mchezo na baadae kuahirishwa.