Waziri Mkuu aagiza kufungwa kwa machimbo ya Boksiti

0
386

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekagua machimbo ya madini ya Boksiti (Bauxite) yaliyopo kwenye eneo la Magamba wilayani Lushoto mkoani Tanga na kuagiza kusitishwa kwa shughuli za uchimbaji katika eneo hilo.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa agizo hilo akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Tanga ambapo alifuatana na Waziri wa Madini Doto Biteko na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angelina Mabula.

Mara baada ya kukagua machimbo hayo ya madini ya Boksiti, Waziri Mkuu amezungumza na Wakazi wa wilaya ya Lushoto katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi ya Mabughani.