Waziri Lukuvi ataka wamiliki wa ardhi walindwe

0
190

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, – William Lukuvi amewaagiza Wakuu wa mikoa kuhakikisha wanawalinda wamiliki wa ardhi ambao wapo kisheria.

Waziri Lukuvi ametoa agizo hilo wilayani Kibaha mkoani Pwani  wakati wa mkutano wa mashauriano baina ya Serikali, Wafanyabiashara na Wawekezaji, mkutano ulioongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, –  Angella Kairuki.

Amesema kuwa, Wakuu wa mikoa wana askari, hivyo wanaweza kuwaondoa watu waliojimilikisha ardhi kinyume cha sheria na kuwataka pia kutumia Mabaraza ya ardhi yaliyoundwa kisheria kuondoa wavamizi kwenye maeneo ambayo yanamilikiwa kisheria.

Wakati wa mkutano huo ambapo Wawekezaji na Wafanyabiashara walipata nafasi kutoa malalamiko yao, Waziri Lukuvi amesema kuwa mkoa wa Pwani ni miongoni mwa mikoa inayoongoza katika uvamizi wa ardhi, huku wilaya ya Bagamoyo ikiwa kinara.