Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu JENISTA MHAGAMA ameuagiza Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi-OSHA, kutaja Ofisi za Serikali ambazo zinaongoza kwa ajali.
Waziri MHAGAMA ametoa agizo hilo Jijini DODOMA katika Mkutano wa Wafanyakazi wa OSHA, ambapo amesema kwa kufanya hivyo kutaiwezesha serikali kuingilia kati na kuzuia ajali hizo.
